Imetundikwa hapa leo hii tarehe 14 Februari, 2013.
TAFAKURI YA KIFO CHA SHEIKH NASSOR BACHO KILICHOTOKEA ZANZIBAR TAREHE 13/2/2013.
Na PAZI MWINYIMVUA
INNA LILLAHI WA INNA ILLAIHI RAJ-UUN.
Mfahamu sheikh Nassor Bachu
Sheikh Nassor Bachu ni miongoni mwa masheikh maarufu ambaye makazi
yake yalikuwa katika visiwa vya zanzibar. Ni miongoni mwa walimu ambaye ana
wanafunzi wengi mno ambao msimamo wao mkubwa ni kufuata na kuhuisha sunna za Mtume Muhammad, Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, amin.
Mchango wake katika jamii
Katika maisha yake alikuwa akitoa darsa zake katika msikiti uliopo
Rahaleo na msikiti wa Kikwajuni Zanzibar. Alipitisha maisha yake yote katika
kufundisha masomo mbalimbali ya dini kama vile tafsiri za quran, hadithi na pia
alikuwa na kipaji cha ziada cha kuzungumza na kueleweka kwa ufasaha. Hivyo pia
ni miongoni mwa watoa mawaidha wazuri sana ambaye kanda zake za mawaidha za redio na za video
zinapatikana katika maduka mingi wanayouza kanda za dini. Pia unaweza kupata
mawaidha yake kwa kupitia www.sekenke.com
au tafuta kwenye www.mawaidha.com
Kwa muda kidogo alipata fardhi ya ugonjwa na hadi kukamilisha
safari ya maisha yake leo siku ya tarehe 13/2/2013.
Nini tutafakari?
Kwanza napenda kunukuu maneno ya Mtume SAW aliposema katika zama
za mwisho wanazuoni wengi watapungua na
maasi yatazidi.
Ni ukweli usiopingika si
rahisi kupata watu wenye ilmu kubwa kama ya sheikh wetu.
Ni wangapi wako tayari kutumia muda wao kutafuta ilmu ya dini kwa
manufaa yao wenyewe sembuse kupata muda wa kuwafundisha wengine?
Ni nani yuko tayari walau kutumia saa chache kwa ajili ya kutafuta
ilmu na kuweza kutumia ilmu hiyo kwa ukweli
namaanisha kwa ikhlasi.
Ibada zetu zimekuwa za
kubabaisha? Kwa kuwa hatuna ufahamu wa kutosha juu ya ibada mbalimbali. Hii ni
kwa sababu hatujajipangia muda wa kuhudhuria katika madrasa na kuweza kupata
ilmu sahihi.
Watoto wetu tumewapangia
program ambazo hawapati hata muda wa kujifunza dini yao na kumjua mtume SAW. Matokeo
yake ni mmomonyoko wa maadili.
Digrii , Masters na PHD zetu zimekuwa ni bure kwani tunashindwa
hata kufanya ibada ya kutafakari na kuweza kuona na kuthibitisha neema za Allah ambazo
amezitaja katika quran pamoja na kuhofishwa na azabu zake. Tumekuwa mstari wa mbele wa kutaja na kueneza aibu za watu kuliko
kuangalia wapi tumekosea na turekebishe.
Hatujiulizi kwa nini? Na mambo haya mpaka lini? Tutaanza kuisoma
dini yetu lini? Masheikh wetu ndugu zangu ndio hao wanamalizika.
Naguswa na msiba huu sana
kwa sifa za kipekee alizonazo Sheikh Nassor Bachu. Machozi hayatasaidia japo
nalo hili huwezi kulizuia.
Mtu mmoja maarufu alisema wakati wa kiza kinene ndio wakati wa
kutafakari na kuweza kuona mwanga. Aristotle. Tafadhali TAFAKARI.
Martin Luther anasema "Laiti kama ningejua kuwa kesho dunia yote
itakatika kuwa vipande basi nisingeacha kupanda mti wa mtufaha". Andaa maisha ya
kesho akhera hata kama u mgonjwa
kitandani au upo kifungoni NA usichoke kupanda mti wa KUTAFUTA ilmu kwani faida zake ni nyingi.
Mtume SAW amesema
Ishi duniani kama utaondoka kesho na ishi duniani kama utabaki
milele. Mihangaiko ya kutafuta maisha ni miongoni mwa sehemu ya dini lakini
iendane na kutafuta maisha ya akhera.
Na Allah SW anasema
Natunawapa muda wa kutosha lakini watambue hakika nguvu yetu ni
kali? Fanya ufanyavo lakini ujue huwezi kushindana na nguvu za Allah.
Pia anasema; Kila binadamu hufanya makosa lakini mbora ni Yule
anaetubia. Tufanye haraka kuomba msamaha na kutorudia makosa.
Katika aya nyingine anasema waja wema wanapofikwa na msiba husema
hakika sisi tunatoka kwa Allah na kwake yeye tutarejea.
Nasi tuseme INNA LILAHI WA INNALAYHI RAJIUN.
1. Ombi langu kwako tafuta kanda yeyote ya mawaidha ya Sheikh Nassor Bachu katika
website nilizozitaja ukurasa wa kwanza ili thawabu ziendelee kumuendea sheikh
wetu na pia uweze kufaidika na ilmu yake.
2. Tumia walau dakika
chache kumuombea dua na kumtakia
msamaha kwa Allah na
amfanyie wepesi wa hesabu zake katika safari ya maisha mapya. Allah alitie nuru na
harufu njema kaburi lake. Amin. Amin
3. Nasi pia tujiombee Allah atupe maisha mema ya duniani na akhera
na atupe mwisho mwema.
No comments:
Post a Comment
BLOGU YA KUWEKA KUMBUKUMBU ZA ASILI ZA WATANZANIA, WAAFRIKA NA WOTE WAZUNGUMZAO LUGHA YA KISWAHILI DUNIANI.