Imeingizwa humu leo hii Jumamosi, tarehe 25/8/2012.
NAOMBA TUZINGATIE YAFUATAYO KUHUSU LUGHA YA KISWAHILI:
1. NI KOSA LA KILUGHA KUSEMA "NI BUDI ..........." KWA MAANA YA
ULAZIMA WA JAMBO FULANI. "BUDI"KATIKA LUGHA YA KISWAHILI INA MAANA YA
"HIYARI", HIVYO UNAPOLITUMIA NI LAZIMA UANZE NA KANUSHO KAMA VILE:
HAPANA BUDI........, SINA BUDI ........... NA KADHALIKA. YAANI " HAPANA
HIYARI.........., SINA HIYARI.
2. NENO "MADHUMUNI" NI NENO LA
KISWAHILI LILILOKOPWA KUTOKA KIARABU. NENO HILI LIPO KATIKA UMOJA NA
"MA" ILIYO MWANZONI MWAKE SI "MA" YA WINGI BALI NI SEHEMU YA NENO
LENYEWE. NI KOSA LA KILUGHA KUSEMA ... "DHUMUNI" BALI SEMA
MADHUMUNI.....
NDUGU YENU,
KHAMIS MATAKA