Friday, August 24, 2012

MWALIMU KHAMISI MATAKA ASAHIHISHA KISWAHILI

 Imeingizwa humu leo hii Jumamosi, tarehe 25/8/2012.
 
NAOMBA TUZINGATIE YAFUATAYO KUHUSU LUGHA YA KISWAHILI:
 
1. NI KOSA LA KILUGHA KUSEMA "NI BUDI ..........." KWA MAANA YA ULAZIMA WA JAMBO FULANI. "BUDI"KATIKA LUGHA YA KISWAHILI INA MAANA YA "HIYARI", HIVYO UNAPOLITUMIA NI LAZIMA UANZE NA KANUSHO KAMA VILE: HAPANA BUDI........, SINA BUDI ........... NA KADHALIKA. YAANI " HAPANA HIYARI.........., SINA HIYARI.
 
 
2. NENO "MADHUMUNI" NI NENO LA KISWAHILI LILILOKOPWA KUTOKA KIARABU. NENO HILI LIPO KATIKA UMOJA NA "MA" ILIYO MWANZONI MWAKE SI "MA" YA WINGI BALI NI SEHEMU YA NENO LENYEWE. NI KOSA LA KILUGHA KUSEMA ... "DHUMUNI"  BALI SEMA MADHUMUNI.....
 
NDUGU YENU,
 
KHAMIS MATAKA

MSEMO WA LEO

 hII IMEINGIA LEO HII  -  Jumamosi tarehe 25 Agosti 2012. 

"Mpe akupaye, ukimpa asiyekupa, ni sawa na kutupa". 

Hii wandugu nimeikuta leo hii Samaki Samaki huko  Mlimani City Shopping Mall,  Dar es Salaam, Tanzania. 

Bado naitafutia methali mlingano wake Kwa Kiingereza.  Tuwe na subira.