Tuesday, August 17, 2010

HUU NDIO UTAMADUNI WA NEPAL

Wandugu,
Hii nimeidaka toka mtandaoni. Nikidhani sisi WAAFRIKA, ndio wanawake tudhalilishwao zaidi kuliko wote duniani, kumbe, kuna wenzetu wametungiwa na tungo kama hizi hapa nilizowatafsiria: (Ukitaka kusoma zaidi tembelea: http://nepaldemocracy.org). Misemo hii pia nimeihifadhi http://tujienzi.blogspot.com

MISEMO YA UDHALILISHAJI WANAWAKE NCHINI NEPAL - 23/3/2010
Imeandikwa na: SAPANA PRADHAN MALLA (http://nepaldemocracy.org)

Beliefs Reflecting the Derogatory Attitude Towards Girl Child/Women including the following:

• Dhilo paye, Chhora paye (“Let it be late, but let it be a son”);
Ni heri kuchelewa kuzaa nipate mtoto wa kiume.

• Chhora paye swarga jaane (“The birth of a son paves the way to heaven”);
Kuzaliwa kwa mtoto wa kiume ni njia ya kuingia peponi.

• Chhori ko janma hare ko karma (“A daughter is born with a doomed fate”);
Mtoto wa kike huzaliwa na mikosi.

• Chhora paye khasi, Chhori paye Pharsi (“If a son is born, it is celebrated by sacrificing a goat, if it’s daughter, a pumpkin is enough”);
Azaliwapo mtoto wa kiume, husherehekewa kwa mbuzi aliyenona, kama ni mtoto wa kike, boga linatosha.

• Chhora bhaye sansar ujyalo, Chhori bhaye bhanchha ujyalo (“Son brightens the whole world, whereas a daughter brightens only the kitchen”);
Mtoto wa Kiume anaangaza dunia nzima, wakati mtoto wa kike anaangaza jikoni tu.

• Kanya Daan (“a daughter should be given away as a gift”);
Mtoto wa kike anastahili kutolewa zawadi tu.

• Mare paap, pale punya (“It’s a sin if the groom kills the bride, charity if nurtured”);
Ni dhambi kwa Bwana harusi kumuuwa bibi harusi, ni huruma tu kwa kumhifadhi.

• Srimati bhaneko paitalako dhulo ho (“Wife is the dust of the foot”);
Mke ni vumbi la nyayoni.

• Chhori mari, thulo ghar pari (“If a daughter dies, we can say she has been married into a rich home”);
Afapo binti, tunaweza kusema kaolewa na tajiri.

• Pothi base ghar mahscha (“A woman ruled house is sure to be destroyed”);
Nyumba itawaliwayo na mwanamke ina hakika ya kusambaratishwa.

• and Swasni mancheko buddhi pachhadi (“Women are always shortsighted”); Wanawake hawana muono wa mbali; wanawake hawaoni mbali.

Sunday, July 4, 2010

UZEE AU U M R I MKUBWA AU KUBOBEA UZOEFU?

Fwd: UzeeFriday, 2 July, 2010 9:11
From: This sender is DomainKeys verified"Saada Al-Ghafry" View contact detailsTo: undisclosed-recipients



Uzee kitu adhimu, huo ninauingia
Ujana sasa adimu, Shabani aliusia
Maungoni mwangu humu, uzee unanijia,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Mbali ninamuachia, rafiki yangu ujana,
Miaka inakimbia, ya leo siyo ya jana,
Nabaki nakumbukia, nilipokuwa kijana
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Shabani aliandika, kaulilia ujana,
Ni vipi unamtoka, kashindwa kuung’ang’ana,
Meno yalimdondoka, na nguvu tena hamna,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Taratibu waingia, uzee wabisha hodi,
Siwezi kuukimbia, hata niwe mkaidi
Hata nikitukania, ndivyo napigwa baridi,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee

Mvi sasa zanijia, nimejaribu kung’oa
Kidevu zasalimia, na miye nazichomoa,
Nikitoa zazidia, nami nazidi kutoa!
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Mapensi nayaachia, na macheni ya shingoni,
Hereni nilivalia, kwenye sikio jamani,
Mwendo nilibadilia, nilivyonesa njiani,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Niliwapata mademu, tena wengine kwa zamu,
Nikaitwa mtaalamu, wa mambo yale matamu
Sasa yanitoka hamu, nanyimwa hata salamu!
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Nilenda nilipotaka, wasiponitaka nilenda,
Sikuwa na hata shaka, ati mtu kunidunda,
Leo naogopa paka, ninavutwa kama punda,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Mwendo wa kudemadema, nikishika natetema,
Uso umenikunjama, natembea nikihema,
Magoti nayo yauma, uzee si lele mama!
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Kumbe maisha ni hivi, uzee haukwepeki,
Ninazikubali mvi, hata kama sizitaki,
Uzee siyo ugomvi, ujana haushikiki,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Kweli nilifurahia, enzi zile za ujana,
Kamwe sintoyarudia, yalopita naagana,
Uzee nakumbatia, kwani lingine hakuna,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Nasubiri wajukuu, nione na vitukuu,
Nakunja miguu juu, na mshukuru Mkuu
Kuona umri huu, enzi hizi ni nafuu,
Na miye nakusalimu, mgeni wangu uzee!

Na. M. M. Mwanakijiji

(Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)

Wednesday, June 9, 2010

FAIDIKA, FARIJIJKA NA KICHEKO! (Enjoy, laugh & cry)!

IMECHANGIWA NA SALIM HIMID WA UFARANSA - 8/6/2010
01
Bi . . . mbona kimya
Hata mwisho wa dunia
Wanitatanya na njia?

02
Si mfu, si kiwete
Si Amani, si Kikwete
Nauguwa kwa matete

03
Yote haya ni ya nini
Ya kunikata maini
Pingu, tazitoa lini?

04
Tazama leo na kesho
Juzi, jana, si kopesho
Yetu, sitie komesho

05
Si Mwarabu, si Mzungu
Si Ngezi, si Takaungu
Nimezengwa, zungu zungu!

06
Kutamani si kupata
Funuwa zako karata
Twende kwa Mparapata!

07
Jozani hata Wete
Wapi Chanda, wapi Pete?
Kiza kaandama Kete

08
Vuga, Shangani, Malindi
Sala zetu za vipindi
Si Tanga wala si Lindi!

09
Chakula kiwe mseto
Ngisi, kambare za peto
Biriani ladha beto

10
Kumbuka Tasi na Changu
Wote ni waja wa M'Ngu
Zohali, Zuhura wangu

11
Bi . . ., mbona kimya?
Si karata, si mpira
Nimezongwa na hasira

12
Hasira, ndugu wa Pwete
Ni suhuba wa Uwete
Wa kuketi pwetepwete!

13
Tutambuwe kwa yakini
Tiba ponesha maini
Iwe Taha na Yasini

14
Tufikapo papo hapo
Pasiwe tena mitapo
Tukumbuke Mkapvapvo!

15
Badamu, ndani mwa kungu
Haivunjwi kwa marungu
Agizo la Bwana M'Ngu

16
Yote haya kuyasema
Tuhudumu yalo mema
Na maovu kuyatema!

17
Pasiwe na tese tese
Za Bwanamkubwa Dese
Na kulala wese wese

18
Fensi hii na ya nini
Ya maua vipinini
Na kuuguza maini?

19
Tufikapo tutakapo
Bandarini ndio hapo
Tujivushe na mitapo

20
Abiria chungu chungu
Jahazi yavunja gungu
Joshi, si wingi utungu!

21
Bi . . ., mbona kimya?
Wingi maji, si maziwa
Titi mama, si za ndiwa

22
Ndiwa usibabaike
Na kutaka ujifiche
Tausi dume, ni mke!

23
Tujipambe kwa majuti
Ya kupigia saluti
Kwa tambavu, si makuti!

24
Hapa wino kaukapo
Ndipo tume ituapo
Yangu risala ikomapo

25
Hala hala pendo langu
Upoleze moyo wangu
Niwe wako, uwe wangu!
____________

S. H.
Paris, France
(+336-27146412)
8th of June 2010.

Wednesday, March 3, 2010

TUIENZI LUGHA YETU ADHIMU YA KISWAHILI

Subject: [www.eThinkTankTz.org], posted on 2 March, 2010.

Maneno Magumu ya Kiteknolojia

We are asking for your help on a quick, important project intended to
improve access to computer technology in East Africa. The task is
simple: look through a list of English terms that are used in
information technology, and vote on the Swahili translations or suggest
your own.

Twaomba msaada wako kwenye mradi muhimu unaolenga kuboresha matumizi ya
teknolojia za tarakilishi katika Afrika ya Mashariki. Shughuli ni
rahisi: tazama orodha ya maneno yanayotumiwa kwenye teknolojia ya habari
na mawasiliano, na kupigia kura tafsiri zilizoko za Kiswahili au
pendekeza neno lako (unalofikiri ni sawa).

We need volunteers with good knowledge of information technology and the
Swahili language. To get started, just visit
https://sites. google.com/ site/manenomagum u

Tunahitaji watu kujitolea ambao wana ujuzi wa teknolojia za mawasiliano
na pia lugha ya Kiswahili. Kuanza, tembelea:
https://sites. google.com/ site/manenomagum u

Several efforts have been made to produce Swahili ICT vocabularies, but
three big problems remain. First, many terms have been given poor
Swahili equivalents because the original concept was misunderstood.
Second, many terms have been given different Swahili equivalents in
different translation projects; the same English term might have five
different Swahili translations, depending on whether you are using
Microsoft, Google, KiLinux, Facebook, or Wikipedia! Third, many terms
have not yet been translated, and new terms keep appearing as ICT
continues to evolve.

Kumekuwepo juhudi mbalimbali za kuandaa istilahi ya teknolojia kwa
Kiswahili, lakini matatizo matatu bado yangalipo. Kwanza, maneno mengi
yalitafsiriwa vibaya kwa sababu ya maana asili kutoeleweka. Pili,
maneno mengi yalitafsiriwa tofauti katika miradi tofauti tofauti ya
utafsiri; inawezekana kuwa neno lile lile la Kiingereza kuwa na tafsiri
tano, kutegemea ikiwa unatumia Microsoft, Google, KiLinux, Facebook, au
Wikipedia! Tatu, maneno mengi hayajatafsiriwa bado, na maneno mapya
yanazidi kuvumbuliwa teknolojia inavyozidi kuwa.

The Kamusi Project is working to harmonize the various "localization"
efforts, in order to have unified, consistent Swahili ICT terminology as
we head into the next decade. Excitingly, we have the encouragement of
both Microsoft and Google, usually big competitors, which are both
interested in greatly expanding access to their services for Swahili
speakers.

Kamusi Project inafanya kazi ya kuunganisha juhudi hizi za
"Uswahilishaji" , ili kuwa na orodha moja inayokubalika, ya istilahi ya
kiteknolojia kwa Kiswahili, tunapoingia enzi ya tarakilishi katika Afika
ya Mashariki. Kinachosisimua ni kwamba tunaungwa mkono na Microsoft na
Google, ambao kwa kawaida ni washindani, ambao wanataka kuongeza sana
huduma zao kwa wanaozungumza Kiswahili.

We have inspected all of the existing ICT terminology lists that we know
of, from which we have produced several "packs" of difficult terms. Now
we are seeking community participation to help reach agreement on how to
express each term in Swahili going forward. The first five packs are
available at https://sites. google.com/ site/manenomagum u

Tumekagua orodha zote zinazopatikana za istilahi ya kiteknolojia, na
tumetayarisha mafurushi kadhaa ya maneno magumu. Sasa tunatafuta jamii
kuchangia ili kufikia makubaliano ya namna ya kusema kila neno kwa
Kiswahili. Mafurushi yapatikana https://sites. google.com/ site/manenomagum u

A few more packs will be added later this week, but we want to start the
community review project immediately so that we can get rapid feedback
if we need to adjust the process. This is an experimental project: as
far as we know, this is the first time that any linguistic community has
invited to help develop the ICT terms that will be used for their
language in the future. If the experiment is successful, we will use
the experience as the basis for more formal terminology development in
the future, for Swahili and other African languages.

Mafurushi mengine machache yataongezwa mwisho wa wiki hii, lakini
tunataka kuanza juhudi hii moja kwa moja ili tupate maoni ya jamii
wanaochangia, kama ni lazima kubadilisha jinsi ya kuendelea. Bidii hii
kweli ni ya majaribio: tunadhani kwamba ni mara ya kwanza kwamba
wasemaji wa lugha yo yote wanakaribishwa kusaidia kwenye maendeleo ya
istilahi ya kiteknolojia itakayotumiwa katika lugha yao. Majaribio
yakifaulu, tutatumia uzoefu huu kama msingi wa maendeleo rasmi zaidi ya
istilahi za kisayansi, kwa Kiswahili na lugha nyingi za Kiafrika.

So, for several reasons, it is very important that we have the
participation of as many people as possible who (a) have a good
understanding of the concepts involved in information technology, and
(b) have good knowledge of the Swahili language.

Kwa hiyo, kwa sababu nyingi, ni muhimu sana tukiwa na watu wengi
watakaojitolea ambao (a) wanaelewa vizuri maswala ya kiteknolojia, na
(b) wanaelewa vizuri Kiswahili.

Please join us, or tell other people who you think might be interested.
The project will end on 7 March, so please contribute this week if
you want your voice to be counted in Swahili localization! Again, the
website is https://sites. google.com/ site/manenomagum u

Twaomba uungane nasi, au ueneze taarifa kwa watu wengine. Juhudi hii
itamalizika 7 Machi, kwa hivyo ni muhimu uchangie wiki hii ikiwa unataka
sauti yako ipate kusikika katika Uswahilshaji wa teknolojia. Tena,
tovuti ni https://sites. google.com/ site/manenomagum u

Notice: this project is only for volunteers who are interested in
promoting the Swahili language. No payments or prizes are available.
This effort is organized by Kamusi Project International
(http://kamusi. org) and ANLoc, and is NOT officially affiliated with
Microsoft, Google, BAKITA, or KiLinux. All suggestions are highly
appreciated, and will be given the most serious consideration in the
production of a harmonized Swahili ICT terminology set that will be made
freely available online within the next few months.

Tangazo: juhudi hii ni kwa watu wa kujitolea wanaotaka kuendeleza
Kiswahili. Hakuna malipo wala tuzo. Bidii hii imepangwa na Kamusi
Project International (http://kamusi. org) na ANLoc, na hauna mahusiano
rasmi na Microsoft, Google, BAKITA, au KiLinux. Tutashukuri kwa
mapendekezo yoyote, na yatafikiriwa sana wakati wa kuandaa istilahi ya
kiteknolojia katika Kiswahili. Istalahi itapatikana bila malipo kwa
wote baada ya miezi michache.

Sunday, February 28, 2010

MOLA MBARIKI MAMA (SHAIRI)

LIMECHANGIWA NA NASRA MOHAMED WA ZANZIBAR
28.2.2010.

M O L A M B A R I K I M A M A

Ya Rabbi Mola Rahima, mwenye kumiliki enzi,
Pokea yangu kalima, ewe usiye na mwezi,
Dua langu nalituma, kwa usiye ni vikwazi,
Mola mbariki Mama, Mama ni wangu kipenzi

Mola mbariki mama, kwa yake bora malezi,
Lolote nitalosema, halitoshi kumuenzi,
Alivyonilea vema, na kunifuta machozi
Mola mbariki Mama, Mama ni wangu kipenzi

Amenifunza hekima, vipi niishi na wenzi,
Na pia bora heshima, nisifate wapotozi,
Hii ni kubwa neema, gizani huwa kurunzi,
Mola mbariki Mama, Mama ni wangu kipenzi

Nilipopigwa na homa, udogoni hizo enzi,
Mama kucha husimama, kwa ule wangu ulizi
Kwa zake nyingi huruma, humiminikwa machozi.
Mola mbariki Mama, Mama ni wangu kipenzi

Kumbatio lake mama, lilinipa utulizi
Kwa sauti yake njema, aliniimbia tenzi
Na kunifunza kusema, mie wake mwanafunzi
Mola mbariki Mama, Mama ni wangu kipenzi

Alinilaza kwa hima, niwapo na usingizi,
Japo awe anahema, kwa kuzidiwa makazi,
Hakika zake huduma, ni pendo lililo wazi,
Mola mbariki Mama, Mama ni wangu kipenzi

Ni nini nimpe mama, kulilipa lake penzi,
Dhahabu kama mlima, ibebwe na wachukuzi,
Haitoshi ninasema, kwa huyu mwema mzazi,
Mola mbariki Mama, Mama ni wangu kipenzi

Beti hii nasimama, bila kufanya mapozi,
Machache niliyosema, mama kumpa pongezi,
Hakika yake karama, kuisahau siwezi,
Mola mbariki Mama, Mama ni wangu kipenzi.

Saturday, February 20, 2010

UTENZI WA WALYD K. HASSAN, DR. YUSSUF S. SALIM, AMANI A. KARUME & MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD

Umeandikwa na Salim Himid (bwanatosha@hotmail.com)
Subject: UTENZI wa Walyd K. Hassan, Dr Yussuf S. Salim, Amani A. Karume & Maalim Seif Sharif (Sehemu 1, 2 & 3)
Date: Wed, 20 Jan 2010 18:39:34 +0000

Sehemu Ya Kwanza

01)-King Walyd mwana wetu
Dokta Yussuf nakwambia
Si mtoto "petu petu"
Lako bora kusikia
Hata uliza Sepetu
Usije potea njia!

02)-Usije potea njia
Wala kupiga mateke
Na kuchanua mikia
Ukapambwa na upweke
Bora tega "kia kia"
Zanzibar isitoweke!

03)-Zanzibar isitoweke
Tutafute itifaki
Du'a zetu tupeleke
Ha Pateli nae Fakih
Mwenye Enzi ndo Mpweke
'Ridhiano kubariki!

04)-'Ridhiano kubariki
Moyo mwema ndio chambo
Pia hayo tusadiki
Tupate kuona mambo
Ifikapo yetu Iddi
Tusije tokwa machango!

05)-Tusije tokwa machango
Angamiza roho zetu
Bora tubane mibango
Kuhifadhi kilo chetu
Amani awe mlango
Na Sefu ndo wimbi letu!

Sehemu Ya Pili

06)-Abdallah Hashim wauzisa
"Blekie bado hajapita?"
ZIRPP, MUWAZA, sisitiza
Sote tusipigwe mateke!

07)-Sote tusipigwe mateke
Yetu zanzibar sitoweke
Zarina, Karama, watete
Naila Majid ndo Rubani!

08)-Naila Majid ndo Rubani
Alipoonja MAGEUZI
Kutuambia tusidhani
Zanzibar ni Kilombero!

09)-Zanzibar si Kilombero
Twache kutiana kero
Yuwapi wetu ndugu Hero
Aje tuvalisha visutu?

10)-Aje tuvalisha visutu
Chankiwiti na mrututu
Farouku nae kuthubutu
Warembo wote kuwavisha!

Sehemu Ya tatu

11)-Yote haya kuongea, kweli ndipo isogee
Ndugu hatujapotea, amani naitokee
Kupenda Zenjibaria, mahaba tutegemee!

12)-Mahaba tutegemee, tusitoswe baharini
Wataka tutokomee, Makamba na mahaini
Msekwa naasekwekwe, 'Ridhiano kubaini!

13)-'Ridhiano kubaini, Miwafaka kwenda pogo
King Hassan haamini, ona watu kwa kisogo
Amani, Sefu, kwa nini, mwatupikia mikogo?

14)-Mwatupikia mikogo, Jussa kuchana viatu
Na tule wetu mhogo, Kikwete apige patu
Amani isende pogo, Zenjibari ina watu!

15)-Zenjibari ina watu, wenye yao tarbia
Uswahili ni ubantu, pamoja na Arabia
Ngazija nao si chatu, Uhindi na Somalia!

Wakatabahu bi-l-yadii,
Salim H. Bwanatosha
(Mngazija wa Zanzibar/Mzenjibari wa Komoro)
Paris, France (+336-27146412)



27
Sefu kupandisha gia
Amani nae kaingia
Wawakilishi wakamavamia
Tulobaki ndo "songa mbele"

28
Tulobaki ndo "songa mbele"
Tujionee ya mabele
Ya Zanzibar hata Mkele
Undugu ndo uwe Jahazi

29
Undugu ndo uwe Jahazi
Kupanda Kusi na Kaskazi
Tusije fanywa wajakazi
Wa majambazi mambo leo

30
Wa majambazi mambo leo
Nchi kufanywa kitoweo
Siasa kuwa ndo uteo
Kuhifadhi yao majungu

31
Kuhifadhi yao majungu
Bila ya kujali M'Ngu
Nchi oneshwa matungu
Rehema itapo wadia?

32
Rehema itapo wadia
Tusiogope kuingia
Tujue yalobakia
Wanaume na wanawake

33
Wanaume na wanawake
Pasiwe alo peke yake
Kula mtu apewe chake
Mseto, choroko na wali

34
Mseto, choroko na wali
Ngoma huchezwa kwa ndzumari
Ndio kuchuma yote mali
Ukweli usiwe na miko

35
Ukweli usiwe na miko
Jinsia iwe hadi mwisho
Kwetu, ungwana ndo mwito
Zanzibar kupandishwa juu

36
Zanzibar kupandishwa juu
Shamhuna hana makuu
Atajipamba Siku Kuu
Na Khatibu kushangiria


37
Na haya yote tunosema
Magazetini tunagema
Fununu papo zinatema
London mkutanoni twende

38
London mkutanoni twende
Tukafichuliwe ya mende
Yasemwao ndani na nde
Maridhiano yawe wazi

39
Maridhiano yawe wazi
Ukweli upate malazi
Kwa Kusi na Kaskazi
Ndo wananchi watakavyo

40
Ndo wananchi watakavyo
Wawakilishi watakayo
Ya kuridhisha Mba Chao
Kwa vishindo na vuguvugu

41
Kwa vishindo na vuguvugu
Tulaani ukorofi sugu
Tupate kufyeka magugu
Kwa kupanta jaha ya tija!

Rendez-vous Abbey Schhol Leisure Centre, Woodbridge Road
Barking, East London
Jumamosi, 13/02/10.

42

Mkutanoni Landani

Sefu keta wake ndani

Kawambia "Ikhiwani

Tusahau yalopita"



43

Tusahau yalopita

Amani mshinda vita

Zanzibar inatuita

Tujihodari kwa yote



44

Tujihodari kwa yote

Tusikose kote kote

Visiwa ni vyetu sote

Tumlaani Shetani!



45

Tumlaani Shetani

Tukinge wetu Watwani

Tujijue sisi nani

Tusitupe Mba Chao



46

Tusitupe Mba Chao

Kwa msala upitao
Shime tuyajue hayo

Zanzibar ipande juu



47

Zanzibar ipande juu

Wirathi wa Mwinyi Mkuu

Pujini hata Bwejuu

Pasiwe waasi tena



48

Pasiwe waasi tena

Mashekhe wamesha nena

Tuhifadhi yalo mema

Tuache ya maferembwe



49

Tuache ya marefembwe

Suluhisho si bwebwe mbwe

Tupanie kwa vibombwe

Ndo chetu kuwa halisi



50

Kuwa na chetu halisi

Kisichokuwa rahisi

Historia yatukisi

Ridhiano ndio ngao



51

Ridhiano ndio ngao

Sote na tujue hayo

Tunapo pambana nao

Wanapopika majungu



52

Wanapopika majungu

Kututia zungu zungu

Kukana amri za M'Ngu

Tunyakue yalokita



53

Tunyakue yalokita

Kwa kujikinga na vita

Mchakato sije sita

Tarakhe kusonga mbele



54

Tarekhe kusonga mbele

Uhai usona ndwele

Sawahil hata Mkelle

Zenjibari ndo johari



55

Zenjibari ndo johari

Wimbi letu la bahari

Iwe ndo kwetu fahari

Ya kucheza mtu kwao



56

Ya kucheza mtu kwao

Aje tunzwa kwa vipao

Tutapike sumu zao

Nchi tena iwe huru



57

Nchi tena iwe huru

Uungwana kuamaru

Muungano uwe nuru

Tujadidi mikataba



58

Tujadidi mikataba

Pwani pamoja na Bara

Tusizongwe na madhara

Tanzania ijiunde



59

Tanzania ijiunde

Bila ya kuliwa kunde

Kwa heshima tuitunde

Uwe muungano wa kweli



60

Uwe muungano wa kweli

Kama bahari na meli

Daftari na jaduweli

Karume na Sefu hawo!

Wakatabahu,

S. H. M. Bwanatosha

London

Jumapili, 14/02/10