TUENZI UTAMADUNI WETU - SHAIRI
Limetungwa na Salim Himidi wa Paris, France.
Chochote kilicho changu,
cha nudhumu na mikeka
Kuhusu mitango yangu,
ya kuliya na kucheka
Moyowe usiwe bangu,
ukachelea kuteka!
Kuteka ni yako haki,
usingiwe na wahaka
Kueneza kulobaki,
zetu mila na baraka
Lugha isije shitaki,
kutokuwa na nyaraka!
Nyaraka ndo zitangao,
walo mbali kuwafika
Wakaribu wajuwapo,
k'wa Jogoo keshawika
Tendeza wajibu wako,
kwa jukumu la Afrika!-----
Afrika ndo Mama/Baba,
chimbuko la binadamu
Tusijione ni wahaba:
wa kuvunja masanamu
Wabaguzi sema kwamba:
HAWA NI WANAHARAMU!
Wasalam, Salim Himidi, Paris, France.
Tuesday, April 14, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
BLOGU YA KUWEKA KUMBUKUMBU ZA ASILI ZA WATANZANIA, WAAFRIKA NA WOTE WAZUNGUMZAO LUGHA YA KISWAHILI DUNIANI.