Imetundikwa hapa leo hii 14.2.2014
NAHAU MPYA ZA KISWAHILI ADHIMU
TUZIINGIZE KWENYE MITAALA YETU?
1. Gari la kuvutwa hali overtake.
2. Hata uwe na bahati vipi hauwezi kuokota nyumba.
3. Mganga wa jadi haagizi samaki/mchicha.
4. Wimbo wa taifa haupigwi disco.
5. Kandambili haipigwi kiwi
6. Usiteme Big G kwa karanga za kuonjeshwa.
7. Hata bibi alikuwa binti.
8. Mke wa mtu sumu, mume wa mtu maziwa.
9. Kipara bila pesa ni kovu.
10. Mbwa hanenepi miguu
11. Picha ya Rais haina bodyguard.
12. Mjini shule kijijini tuition.
13. Uzuri na shepu mjini, tabia kijijini
14. Mjini heshima pesa, shikamoo makelele.
15. Silaha pesa, kisu na bastola mizigo.
16. Kuku ni kuku tu, jogoo jina.
17. Kusoma kuelewa kukesha mbwembwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
BLOGU YA KUWEKA KUMBUKUMBU ZA ASILI ZA WATANZANIA, WAAFRIKA NA WOTE WAZUNGUMZAO LUGHA YA KISWAHILI DUNIANI.