Saturday, February 16, 2013

NAHAU MPYA ZA LUGHA YA KISWAHILI TANZANIA !!!!

Imetundikwa hapa leo hii  tarehe  17/2/2013.

NAHAU  HIZI ZIMEDAKWA  KUTOKA  MTANDAONI   TANZANET !!!!

Pesa hainunui ustaarabu.


Mshamba utampeleka mjini ila ushamba kuuondoa kazi.

Gari alilopanda yesu, shetani haombi lifti.

Gari la kuvutwa haliovateki (overtake)

Hata uwe na bahati vipi,  huwezi kuokota nyumba.

Mganga wa jadi haagizi samaki wala mchicha.

Wimbo wa taifa haupigwi disco.

Kandambili haipigwi kiwi.

Usiteme Big G (chewing gum) kwa karanga za kuonjeshwa.

Hata bibi alikuwa binti.

Mke wa mtu sumu, mume wa mtu maziwa.

Kipara bila pesa ni kovu.

Mbwa hanenepi miguu.

Picha ya Rais haina Mlinzi (bodyguard).
Mjini shule,  kijijini tuition.

Uzuri na shepu mjini, tabia kijijini.

Mjini heshima pesa, shikamoo makelele.

Silaha pesa, kisu na bastola mizigo.

Kuku ni kuku tu, jogoo jina.

Kusoma kuelewa kukesha  ni mbwembwe  tu.

Ukitafuta heshima kwa gharama utauziwa fedheha kwa bei nafuu.





5 comments:

BLOGU YA KUWEKA KUMBUKUMBU ZA ASILI ZA WATANZANIA, WAAFRIKA NA WOTE WAZUNGUMZAO LUGHA YA KISWAHILI DUNIANI.