Monday, January 12, 2015

NAHAU ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE [TRANSLATED SWAHILI SAYINGS]

Imenukuliwa kutoka Gazeti la HABARILEO, Tanzania la Alhamisi,  Januari 8 - 14, 2015
Na  GENOFEVA  MASAO

Amekula chumvi nyingi            -  Ameishi miaka mingi [lived a long life]
Ahadi ni deni                           - Timiza ahadi yako [be trustworthy; keep your promise]
Amewachukua wazee wake    -  Anawatunza vizuri wazazi wake [taking good care of parents]
Amekuwa popo                      - Yu kigeugeu [ a turncoat]
Amevaa miwani                      - Amelewa pombe [chakari] [inebriation, a drunkard]
Amekuwa mwalimu                 - Yu msemaji sana  [a talkative person]
Amemwaga unga                     - Amefukuzwa kazi [ dismissed from employment]
Ana ulimu wa upanga               - Ana maneno makali  [biting words]
Ameongezwa unga                  - Amepandishwa cheo [promoted]
Agizia risasi                             - Piga risasi  [shoot!]
Chemsha bongo                      - Fikiri kwa makini  [think analytically]
Kuchungulia  kaburi                 - Kunusurika kifo   [saved from a worse fate]
Fyata mkia                              - Nyamaza [keep silent]
Fimbo zimemwota mgongoni    -Ana alama ya mapigo ya Fimbo mgongoni [birching scars on ones' back]
Hamadi kibindoni                    - Akiba iliyopo kibindoni [savings for a rainy day]
Hawapikiki chungu kimoja       -Hawapatani kamwe !  [always at loggerheads]
Kupika majungu                      - Kufanya mkutano wa siri [conspire a secret meeting]
Kumpiga [kumvika] kilemba cha ukoka   -  Kumsifu mtu kwa unafiki [kinafiki] [paying lip service]
Kula mlungula                          - Kula rushwa [receiving a bribe]
Kupelekwa miyomboni            - Kutiwa [kupelekwa] jandoni [performing circumcision]
Kujipalia mkaa                         - Kujitia matatani [get yourself in trouble]
Kumeza [zea] mate                  - Kutamani   [to crave for]
Kumuuma mtu sikio                 - Kumnong'oneza mtu jambo la siri [tell a secret to someone]
Kumpa nyama ya ulimi             -Kumdanganya mtu kwa maneno matamu [using wiles to tell lies]
Kumchimba mtu                      - Kumpeleleza mtu siri yake  to dig one's secrets]
Kutia chumvi  katika mazungumzo  -  Kuongea habari za uwongo [tell lies]
Vunjika moyo                          -  Kata tamaa [give up]
Yalimkata maini                       - Yalimtia uchungu  [emotional pain]
Kujikosoa                               - Kujisahihisha  [correct your ways]
Kutia utambi                            - Kuchochea ugomvi  [convince someone to fight]
Kumeza maneno                      - Kutunza siri moyoni  [to keep a secret]
Kula njama                              - Kufanya mkutano wa siri [to conspire a secret meeting]
Kumkalia mtu kitako                - Kumsema/kumsengenya  [to talk about someone]
Kupiga vijembe                        - Kumsema mtu kwa fumbo [use idioms to talk about someone]
Kiinua mgongo                         - Malipo ya pongezi/uzeeni [pension]
Kazi ya majungu                       - Kazi ya kumpatia mtu posho [hand to mouth existence]
Kaza kamba                             - Usikate tamaa - [never give up!]
Kumwonyesha mgongo             -  Kujificha - [to hide]
Kuona cha mtema kuni             -  Kupata mateso [torture]
Maneno ya uwani                     - Maneno yasiyo na maana/porojo  -  [hyperbole !]
Mate ya fisi                              -  Kata tamaa kupita kiasi - [give up totally !]
Mbiu ya Mgambo                     - Tangazo [advertisement]
Mungu amemnyooshea kidole   - Mungu amemuadhibu -  [God's punishment]
Mkubwa jalala                          - Kila  lawama hupitia kwa mkubwa - [The eldest is the Dumping ground!]
Mkaa jikoni                               - Mvivu wa kutembea -  [a stay at home person]
Mungu si Athumani                    - Mungu hapendelei [God is fair]
Ndege mbaya                            - Bahati mbaya [bad luck]
Paka mafuta kwa mgongo wa chupa - Danganya [telling lies]
 Usiwe kabaila                                  - Usichume tokana na jasho la mwingine [Don't exploit others]
Usiwe kupe                                      -  Fanya kazi [be gainfully employed]
Usiwe bwanyenye                             -  Usichume kwa vitega uchumi vyako [don't be a capitalist!]
Usiwe na mrija                                  -  Usinyonye wenzako  [don't be exploitative]
Utawala msonga                               - Utawala wa wachache [leadership of the few]
Usiwe nyang'au                                 - Usidhulumu kwa kutumia madaraka [Don't use your position to exploit others]
usiwe Kikaragosi                              -  Usiwe chui katika ngozi ya kondoo [Don't be a sheep in a leopard's skin]
Umangimeza                                     -  Viongozi wanaopenda kuamrisha watu [a Dictatorship]
Kutoa ya mwaka                               - Kufanya jambo zuri na la pekee [performing a unique act]
Kumpa mtu ukweli wake                  -  Kumwambia mtu wazi [to be transparent]
Pua kukaribiana kushikana na uso     -  Kukunja uso kwa hasira [to express anger]
Sina hali                                            - Sijiwezi  [I am helpless (mostly when talking about love)]
Kupiga uvivu                                     - Kukaa tu bila kazi [abject laziness]
Kupiga kubwa                                   -  Kwenda moja kwa moja [vanishing act]
Kumwekea mtu deko                         -   Kulipiza  kisasi [pay back]
Mtu mwenye ndimi mbili                     -  Kigeugeu  [A turncoat]
Miamba ya mitishamba                       - Wanga hodari wa kienyeji [ expert wizardry]
Kupiga supu                                       - Tegea  [do the least]
Kupiga mali shoka                              - Gawana  [distribute (contraband, bullion, inheritance]
Kula vumbi                                         - Pata taabu   [struggle]
Mafungulia ng'ombe                            - Kati ya saa mbili na saa tatu [between 8.00  and 9.00 o'clock
Kutia kiraka                                        - Fichia siri [confiante]
Kumlainisha mtu                                  -  Kumzungumzia mtu maneno matamu mpaka akubali matakwa yako [convince someone to see eye to eye - to agree to your argument]
            






85 comments:

  1. Shukuran, jazaaka Allaahu khayra

    ReplyDelete
  2. Shukuran, jazaaka Allaahu khayra

    ReplyDelete
  3. Naamini nitaelewa nikizingatia vyema

    ReplyDelete
  4. asante sana. kazi yako ni nzuri

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  6. hhhhxggh1cfdytf35GDFYVVbf3ysgyfd5VSD53Fdyefv3f

    ReplyDelete
  7. Asante.
    Naomba kujua maana ya Toa wosia, askari kanzu na kichogo

    ReplyDelete
  8. inapendeza sanaaa,, nimefurahia sana

    ReplyDelete
  9. Naomba kujua maana ya najua hizi
    1. Ona sifa

    2. Moyo mweupe

    ReplyDelete
  10. Naomba kujua maana ya anapiga pasi na amepiga mbio

    ReplyDelete
  11. Replies
    1. Asante sana kwa kazi nzuri umeniweka safi sana kwa nahau zako mungu azidi kukufunulia

      Delete
    2. Nataka kujua maana ya nahau kata maini,piga chenga,kaza roho,fungasha virago na moyo mkunjugu

      Delete
  12. Nini maana ya nahau. Kwenda joshi?

    ReplyDelete
  13. Naomba kujua maana ya kula mwata,pigwa kalamu,kunoa lubu

    ReplyDelete
  14. Maana ya nahau “mtoto wa kikopo”

    ReplyDelete
  15. maana ya nahau kuuponda wa fisi msaada please

    ReplyDelete
  16. Replies
    1. piga mbiu ni kutoa sauti ya kuonyesha hatari

      Delete
  17. Nini maana ya nahau ya mtu aliyejitakia jambo

    ReplyDelete
  18. Nahau ipi ya mtu aliyejitakia jambo

    ReplyDelete
  19. Nini maana ya nahau tia nanga,kufa kishujaa na kata maini

    ReplyDelete
  20. namba msaada, kula kikoa maana yake nini

    ReplyDelete
  21. Naomba maana ya nahau kula kadhongo

    ReplyDelete
  22. 1. Nahau ya Ana inda?
    2. Linda doria?

    ReplyDelete
  23. Maana ya kuvishwa kilemba Cha ukoka


    ReplyDelete
  24. Nini maana ya kubali kwa ulimi?

    ReplyDelete
  25. Nini maana ya nahau mtu kidole

    ReplyDelete
  26. Kufa kishujaa maana yake ni nini?

    ReplyDelete
  27. Naomba kujua maana ya piga maji

    ReplyDelete
  28. Naomba maana ya nahau hizi,noa Ulimi,kuwa kasuku,roho kwenda just,fuja mipango,ota manyoya,kalia kuti kavu,ponda mali,ndimi kali

    ReplyDelete
  29. Maana ya nahau anamiraba minne,toa heshima

    ReplyDelete
  30. Samahani nini maana ya nahau hizi. Kufa moyo,kata roho ,Kara shauri ,lala tanga ,chapa mguu

    ReplyDelete
  31. Samahani Nini maana ya kufa kiofisa?

    ReplyDelete
  32. Nini maana ya nahau kula ngwaba

    ReplyDelete
  33. Maana ya nahau noa ulimi ni ipo?!

    ReplyDelete
  34. nini maana ya nahau "ota manyoya"

    ReplyDelete
  35. Mtu ambaye ni mgeni mahali fulani na anayeonesha tabia tofauti na wenyeji wake.

    ReplyDelete

BLOGU YA KUWEKA KUMBUKUMBU ZA ASILI ZA WATANZANIA, WAAFRIKA NA WOTE WAZUNGUMZAO LUGHA YA KISWAHILI DUNIANI.